Home Uncategorized MUANGOLA WA YANGA ALIGOMA KWENDA KUCHEZA ULAYA, KISA YANGA

MUANGOLA WA YANGA ALIGOMA KWENDA KUCHEZA ULAYA, KISA YANGA


 IMEELEZWA kuwa kiungo mshambuliaji wa Yanga raia wa Angola, Carlos St’enio Fernandez ‘Carlinhos’,  amekataa ofa ya kwenda kucheza soka la kulipwa Ureno na badala yake ameamua kuja kukipiga Jangwani.

 

Yanga chini ya wadhamini wao Kampuni ya GSM, hivi karibuni ilifanikisha usajili wa mshambuliaji huyo aliyekuwa anakipiga Interclube ya nchini Angola kwa ajili ya msimu ujao.

 

Kwa mujibu wa Injinia  Hersi Sai , ujio wa mshambuliaji huyo Yanga umewashtua watu wengi Angola, kwani walitarajia kumuona akienda kucheza soka Ureno.

 

“Ujio wa Carlinhos hapa Yanga umewashtua wadau wengi wa soka nchini Angola, kwani wengi walitarajia kumuona akienda kucheza soka Ulaya na siyo Yanga.

 

“Hiyo ni kutokana na kiwango kikubwa ambacho anacho hivi sasa kwani ni kati ya wachezaji nyota wanaotazamwa Angola.  Amekataa ofa ya kwenda kucheza soka la kulipwa Ureno,” alisema Hersi.


Nyota huyo kwenye kilele cha Wiki ya Mwananchi, Uwanja wa Mkapa alitumia dakika 9 uwanjani kuonyesha makeke yake kwenye mchezo wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya Aigl Noir.


Yanga ilishinda kwa mabao 2-0 kwenye mchezo huo ambapo mabao yalifungwa na Michael Sarpon na Tuisila Kisinda.


Tamasha hilo lilikuwa na mvuto wa kipekee na lilipokelewa kwa utofauti na mashabiki wengi ambao walijitokeza uwanjani.


Ofisa Uhamasishaji wa Yanga, Antonio Nugaz amesema kuwa kwa namna mashabiki walivyojitokeza wanastahili shukrani na kuwaomba waendelee kuipa sapoti timu yao bila kuchoka.

SOMA NA HII  MAPROO WAWILI SIMBA KUKUTANA NA BALAA ZITO, KAGERE NDANI