Home Uncategorized NGASSA HUYO KUKIPIGA NDANI YA NDANDA FC

NGASSA HUYO KUKIPIGA NDANI YA NDANDA FC

 


KIUNGO mkongwe ndani ya Bongo aliyekuwa anakipiga ndani ya Klabu ya Yanga inaelezwa kuwa msimu ujao atakuwa ndani ya Klabu ya Ndanda FC inayoanza safari yake ya kusaka tiketi kurejea ndani ya Ligi Kuu Bara.


Ndanda ni miongoni mwa timu ambazo zilishuka daraja msimu wa 2019/20 baada ya kumaliza ligi ikiwa nafasi ya 19 na pointi zake 41 baada ya kucheza mechi 38.


Nyingine ambazo zilishuka ni pamoja na Alliance FC na Mbao FC zote za Mwanza, Singida United ilianza kukata tiketi mapema na Lipuli FC ya Iringa nazo zitashiriki Lig Daraja la Kwanza.


Taarifa kutoka kwa mtu wa karibu wa Ngassa imeeleza kuwa:”Ngassa anarudi kwenye timu yake ya zamani Ndanda ambayo aliicheza kabla ya kuibukia ndani ya Yanga.”

Julai 26, Ngasa alitoa pasi yake ya mwisho kwa David Molinga raia wa Congo mbele ya Lipuli, Uwanja wa Samora ambao hawa kwa pamoja hawatakuwa ndani ya kikosi cha Yanga baada ya mikataba yao kuisha. Nyota wengine ambao wameibukia ndani ya Ligi Daraja la Kwanza ambao watakipiga ndani ya Ndanda ni pamoja na Luccian William ambaye mkataba wake ndani ya Polisi Tanzania ulikwisha.

SOMA NA HII  BALINYA AMWAGIWA NOTI ZA MAANA YANGA, MIFEDHA MINGINE KUTOLEWA