Home kimataifa HII HAPA HOTUBA YOTE YA MESSI AKIAGA BARCELONA

HII HAPA HOTUBA YOTE YA MESSI AKIAGA BARCELONA


MSHAMBULIAJI wa klabu ya Barcelona, Lionel Messi leo Jumapili asubuhi alishindwa kujizuia na kujikuta akitokwa na machozi wakati akiwaaga wachezaji, viongozi na mashabiki wa Barcelona, huku tetesi zikieleza kuwa anaelekea PSG.

Akiwa anabubujikwa na machozi katika mkutano huo Messi amesema: “Maisha yangu yote, bado nahisi sipo tayari kwa hili. Mwaka huu mimi na familia yangu tulifikia uamuzi wa kusalia hapa licha ya hapo awali kuleta barua ya kutaka kuondoka.

“Muda tuliokuwa nao hapa umekuwa bora sana, lakini leo ninalazimika kusema kwaheri kwa haya yote, nimekuwepo hapa tangu nikiwa na miaka 13, na baada ya miaka 21 naondoka na mke wangu na vijana wangu watatu.

“Sishawishiki kusema kuwa sitarejea tena, lakini nashukuru sana kwa kila kitu, kwa wachezaji wenzangu na ambao nimewahi kucheza nao hapa nawashukuru sana, licha ya kwamba wengine tulikutana kwa muda mchache.

“Nimekutana na mambo mengi mazuri, na machache ambayo yalikuwa changamoto kwangu ambayo yalinifanya nijifunze na kukua zaidi kufikia nilipo sasa, naamini nilijitolea kila kitu kwa klabu hii na jezi hii kuanzia siku ya kwanza mpaka mwisho.

“Ukweli ni kwamba ninaondoka, licha ya kwamba sikuwahi kufikiri kama kuna siku ningewaaga, ninatamani ningeweza kutamka maneno haya mbele ya mashabiki waliojazana kwenye uwanja huu, lakini kwa bahati mbaya haijawa hivyo.”

SOMA NA HII  DUUH! CHEKI JUMBA HILI LA KIFAHARI LA RONALDO...LAPANGISHWA MAMILIONI KWA MWEZI