Home Simba SC JEMBE JIPYA SIMBA LAANZIA ‘GYM’

JEMBE JIPYA SIMBA LAANZIA ‘GYM’


BAADA ya kukamilisha usajili wake wa kujiunga na Simba, aliyekuwa mshambuliaji wa Mbeya City, Kibu Denis sasa ameanza na programu maalum ya mazoezi ya Gym kwa ajili ya kujiweka sawa kuelekea msimu ujao wa 2021/22.

Inaelezwa kuwa tayari Kibu amekamilisha kila kitu na Simba kwa ajili ya kuwatumikia msimu ujao, na sasa anasubiri kutambulishwa rasmi kwa Wanasimba ili aanze kukitumikia kikosi hicho.

Kibu amesajiliwa Simba kama pendekezo la kocha mkuu wa klabu hiyo, Didier Gomes ambapo anakuja kuongeza nguvu kwenye safu ya ushambuliaji ya timu hiyo, ambayo inatajwa iko kwenye mpango wa kuachana na straika mmoja.

Akiwa na Mbeya City Kibu msimu uliopita Kibu alifanikiwa kuonyesha uwezo mzuri kiasi cha kuhusika kwenye zaidi ya mabao manne, na kupata nafasi ya kuitwa kwenye kikosi cha timu ya Taifa kilichocheza dhidi ya Malawi.

Kuhusu usajili wake Kibu amesema: “Nipo Dar es Salaam kwa ajili ya kukamilisha usajili wangu kwenye klabu moja kubwa, tuendelee kusubiri kila kitu kitawekwa wazi hivi karibuni.”

SOMA NA HII  GOMES - MATOKEO YA JUMAMOSI YAMETUUMIZA MNO