Home Simba SC HAWA HAPA WAWILI WANATAJWA KUBEBA MIKOBA YA SVEN NDANI YA SIMBA

HAWA HAPA WAWILI WANATAJWA KUBEBA MIKOBA YA SVEN NDANI YA SIMBA

 MAJINA mawili ya makocha wakubwa yamekuwa yakipewa nafasi ya kuibuka ndani ya kikosi cha Simba kuchukua mikoba ya Sven Vandebroeck ambaye alibwaga manyanga Januari 7.

Vandebroeck raia wa Ubelgiji kwa sasa yupo zake nchini Morocco akiwa na timu mpya huku akisepa Simba kwa kile ambacho alieleza kuwa ni matatizo ya kifamilia.

Kwa sasa timu ipo chini ya Kaimu Kocha Mkuu, Seleman Matola ambaye alikiongoza kikosi hicho kutiga hatua ya fainali ya Kombe la Mapinduzi ila akapoteza kwa kufungwa kwa penalti 4-3 baada ya dakika 90 kukamilika kwa sare ya bila kufungana.

Habari zimeeleza kuwa mrithi wa Sven ambaye anaifundisha timu ya FAR Rabat kwa sasa atatangazwa muda wowote kuanzia sasa kwa kuwa viongozi walikuwa wanasubiri Kombe la Mapinduzi liishe.

“Kombe la Mapinduzi lilikuwa linachelewesha kutangazwa kwa kocha mpya, tayari majina yalichaguliwa na wengine saba ambao walipita walikutana na Mtendaji Mkuu,(CEO) kwa ajili ya usaili.

“Majina ambayo yanatajwa sana ni pamoja na Florent Ibenge ambaye ni Kocha Mkuu wa AS Vita ya Congo pamoja na Rene Weiller ambaye amewahi kuifundisha Al Ahly ya Misri.

“Ila sasa kinachositisha dili la huyo Rene ni mkwanja kwani anahitaji fedha ndefu hivyo ikiwa mazungumzo yataeleweka anaweza kuwa mrithi wa mikoba ya Sven,” ilieleza taarifa hiyo.

Mtendaji Mkuu wa Simba, Barbara Gonzalez amesema kuna CV zaidi ya 50 ambazo zilitumwa na zimefanyiwa kazi ila katika CV hizo hakuna Mtanzania hata mmoja.

Ibenge akizungumzia dili lake la kujiunga na Simba aliweka wazi kwamba waliwahi kumfuata wakihitaji huduma yake.

“Sio Simba pekee hata Yanga na Azam pia zimekuwa zikitajwa kuhitaji huduma yangu, zote ninazihesimu ila kwa sasa nipo na AS Vita tusubiri na tuone,”.

SOMA NA HII  SIMBA YAPELEKWA MAHAKAMANI NA RWEYEMAMU