Home Ligi Kuu VIUNGO WAWILI WA MTIBWA SUGAR WAREJESHA MATUMAINI

VIUNGO WAWILI WA MTIBWA SUGAR WAREJESHA MATUMAINI

 


VIUNGO washambuliaji wa Klabu ya Mtibwa Sugar, Haruna Chanongo na Salum Kihimbwa wamerejesha matumaini kwenye kikosi hicho baada ya kupona majeraha yao.

Kwenye msimamo wa Ligi Kuu Bara, Mtibwa Sugar ipo nafasi ya 15 na mwendo wake unaonekana kuwa wa kusuasua.

Nyota hao wawili walikuwa wanasumbuliwa na majeraha ya misuli waliyopata jambo lililowafanya wake nje ya uwanja kwa muda mrefu.

Kaimu Kocha Mkuu wa Mtibwa Sugar, Vincent Barnabas alisema kuwa nyota hao walianza mazoezi mepesi mwishoni mwa wiki iliyopita. 

Barnabas alisema kurejea kwa viungo hao kutaimarisha kikosi chake katika safu ya kiungo ambayo hivi sasa inachezwa na Baraka Majogoro na Jaffar Kibaya.

“Habari njema kwa mashabiki wa Mtibwa Sugar ni kuwa viungo wao Kihimbwa na Chanongo wiki iliyopita walianza mazoezi mepesi ya binafsi kabla ya wiki ijayo kuanza kuanza mazoezi magumu.

“Viungo hao walikosekana kwa muda mrefu katika kikosi changu kutokana na majeraha hivyo ninafurahi kuwaona wakirejea uwanjani,” 

SOMA NA HII  RUVU SHOOTING YATEMBEZA 5G BONGO