Home Yanga SC VIGONGO VYA YANGA KWA LIGI HIVI HAPA IKIMALIZA INAKUTANA NA SIMBA

VIGONGO VYA YANGA KWA LIGI HIVI HAPA IKIMALIZA INAKUTANA NA SIMBA


BAADA ya kumalizana na KMC kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara, juzi Aprili 10, Uwanja wa Mkapa na ubao kusoma Yanga 1-1 KMC, vinara hao wa ligi wana vigongo vingine vitatu wakimalizana na hivyo watakutana na Simba.

Kwenye msimamo ipo nafasi ya kwanza ikiwa na pointi 51 imecheza jumla ya mechi 24 msimu wa 2020/21

Aprili 17 ni Yanga dhidi ya Biashara United ya Mara, Uwanja wa Mkapa.

Mzunguko wa kwanza walipokutana Uwanja Karume ngoma ilikuwa Biashara 0-1 Yanga.

Aprili 20 ni Yanga dhidi ya Gwambina FC, Uwanja wa Mkapa.

Mchezo wa kwanza walipokutana Uwanja wa Gwambina Complex ubao ulisoma Gwambina 0-0 Yanga.

Aprili 25 ni Yanga dhidi ya Azam FC, Uwanja wa Mkapa.

Walipokutana Uwanja wa Azam Complex ubao ulisoma Azam FC 0-1 Yanga.

Dabi yao itakuwa ni Mei 08 Simba dhidi ya Yanga, Uwanja wa Mkapa. Ile iliyopita ilikuwa Yanga 1-1 Simba.

SOMA NA HII  HAO YANGA WASIKIENI TU HIVYO HIVYO...KAZE AANIKA BALAH JIPYA...WAITAJA SIMBA...