Home Habari za michezo SIKU CHACHE BAADA YA KUMPA MSAMAHA…SIMBA WAAMUA ‘KUJIMALIZA MAZIMA’ KWA CHAMA….

SIKU CHACHE BAADA YA KUMPA MSAMAHA…SIMBA WAAMUA ‘KUJIMALIZA MAZIMA’ KWA CHAMA….

Habari za Simba SC

KLABU ya Simba imeshtuka, na sasa imeamua kumuandaliwa mkataba mnono kiungo wao Clatous Chama ambao unaelekea ukingoni.

Awali kulikuwa na taarifa kuwa kiungo huyo angeweza kuachwa mwishoni mwa msimu kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo utovu wa nidhamu, lakini kiwango alichoonyesha katika mechi dhidi ya Mashujaa FC na juzi dhidi ya Tabora United, kimewafanya viongozi wa Simba na Kocha Mkuu, Abdelhak Benchikha kupagawa na kukaa chini kumuandaliwa mkataba mwingine mnono.

Katika mchezo wa juzi kiungo huyo aliweza kuchangia mbao mawaili katika timu yake ya Simba dhidi ya Tabora United kwa kuibuka na ushindi wa mabao 4-0, uwanja wa Al Hassan Mwinyi, uliopo Tabora, ukiwa mchezo wa Ligi kuu Tanzania Bara.

Taarifa za uhakika zilizoifikia kuwa uongozi wa Simba uko kwenye mipango ya kumuongezea mkataba mpya Kiungo huuo baada ya ule wa awali kufikia tamati kwa kubakiza miezi sita ili ufike tamati.

Mtoa habari huyo amesema hatua ya kumuongezea mkataba nyota huyo ni baada ya mazungumzo ya pande zote ikiwemo benchi la ufundi linaloongozwa na Abdelhak Benchikha juu na uongozi.

“Suala la usajili lazima kocha ashirikishwe iwe nyota wapya na hata wale mikataba yao ipo ukingoni inakaribia kufikia tamati, akiwemo Chama ambaye amebakiza miezi sita ili awe huru ni miongoni mwa nyota ambaye anajadiliwa kwa ajili ya kuongezewa mkataba mwingine kutumikia misimu mingine,” amesema kigogo huyo.

Chama amesema bado ni mchezaji halali wa Simba ana mkataba wa miezi sita, suala la kuongeza hilo anaamini ni suala lipo kwa uongozi wake kikubwa anafurahia kuona amekuwa sehemu ya kuchangia ushindi wa timu hiyo.

“Ushindi mzuri kwa timu kwa kuondoka na pointi tatu muhimu dhidi ya Tabora United, nina furaha kuchangia moja kwa moja mabao mawili na kufika malengo yetu ya kupata alama tatu katika mchezo huo,” amesema kiungo huyo.

SOMA NA HII  ALICHOSEMA ROBERTINHO KUHUSU SARR.....AGUSIA ISHU YA SIMBA....