Home Habari za michezo BAADA YA ‘KUIGODOA’ DODOMA JUZI…’SHOW’ ZA GAMONDI SASA ZINAHAMIA HUKU….

BAADA YA ‘KUIGODOA’ DODOMA JUZI…’SHOW’ ZA GAMONDI SASA ZINAHAMIA HUKU….

Habari za Yanga leo

MABINGWA Watetezi na vinara wa Ligi Kuu, Yanga, kesho wanashuka dimbani kusaka pointi tatu muhimu dhidi ya wageni wao, Mashujaa FC katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara, uwanja wa Azam Complex uliopo Chamazi, Dar es Salaam.

Katika mchezo huo kila mmoja anahitaji alama tatu muhimu kwa ajili ya kujiweka katika mazingira mazuri ya msimamo huku Yanga akijihakikisha anaendelea kushika usukani na Mashujaa FC inajinasua kutoa chini ya msimamo.

Wakati Yanga inaongoza ligi ikiwa na pointi 34 wanakutana na Mashujaa FC iliyopo nafasi ya 15 yenye alama 19. Katika mechi za mwisho Wananchi walipata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Dodoma Jiji FC huku Mashujaa FC wakipoteza mechi yao ya ugenini na Simba.

Yanga itaendelea kumkosa nyota wake winga, Agustino Okrah bado hajawa fiti, alipata maumivu kwenye mchezo wake wa kwanza kuvaa uzi wa Yanga katika mechi za ushindani ilikuwa Mapinduzi 2024, Zanzibar.

Hakuwa sehemu ya kikosi kilichocheza mchezo wa kwanza ndani ya Februari 2 Uwanja wa Kaitaba Kagera Sugar 0-0 Yanga ikiwa ni sare ya kwanza, Dodoma Jiji FC.

Kuelekea mchezo huo Kocha Miguel Gamondi amesema wamefanya maandalizi kwa ajili ya mchezo wa kesho kuhakikisha wanaendelea kupata matokeo mazuri na kuendelea kuongeza katika msimamo.

Amesema anatambua mchezo hautakuwa rahisi kwa sababu ya wapinzani wao kutoka kupoteza mechi na wanahitaji alama kama ilivyo kwao ili kujiweka kwenye mazingira mazuri ya mipango yao.

“Hii ratiba ni kwa timu zote, kikubwa ni kufanya maandalizi kwa ajili ya mchezo huo kwa kuwajenga kisaikolojia wachezaji wetu, haitakuwa mechi rahidi kwa sababu ya wapinzani wetu nao wamejipanga kuleta ushindani mkubwa,” amesema Gamondi.

Kocha Mkuu wa Mashujaa FC, Mohammed Abdallah ‘Bares’, amesema mchezo kubwa kwao katika soka sio kubwa kwa sababu wote wanacheza 11, wamejiandaa vizuri kwa ajili ya kutafuta matokeo chanya.

Amesema wanaenda kuheshimu Yanga kwa sababu timu ina wachezaji wengi wametoka katika michuano ya kimatiga lakini ya kuwa na wachezaji ambao hawashiriki michuano hiyo lakini wanaenda kupambana kusaka alama muhimu.

“Ugumu uliopo ni jografia yetu ya nchini lakini hakuna presha yoyote juu ya kutoka kwenye mechi ngumu na Simba na sasa tunaenda kukutana na timu kubwa, dhidi ya Yanga, kikubwa tunaenda kufanya vizuri na kutorudia makosa.

Cha muhimu kwetu ni matokeo hatuangaliii tunaenda kucheza na timu yenye ukubwa gani, kikubwa tumefanya maandalizi mazuri kukabiliana na Yanga katika mchezo wetu wa leo,” amesema Bares.

Mwakilishi wa wachezaj Mashujaa FC, Baraka Mtui amesema maandalizi mazuri na kuhakikisha hatawaangusha mashabiki wao na watu wa Kigoma, kwa kuwapa furaha baada ya kupoteza mechi uliopita.

“Tulipoteza mechi na Simba ni timu kubwa na tunaenda kukutana na Yanga nao wakubwa lakini tumejipanga na tutacheza kwa kuwaheshimu na kufuaya maelekezo tuliyopewa na benchi la ufundi,” amesema Mtui.

SOMA NA HII  MSEMAJI AZAM FC AJIINGIZA KWENYE LIGI YA UBISHANI KUHUSU UWEZO WA MORRISON....ADAI HANA UBORA WOWOTE...