Home Habari za michezo NATAMANI ULE MOYO WA UPAMBANAJI WA KIBU DANIS NIUONE KWA WACHEZAJI WOTE...

NATAMANI ULE MOYO WA UPAMBANAJI WA KIBU DANIS NIUONE KWA WACHEZAJI WOTE WA SIMBA KULE CAIRO..

Habari za Simba

Ukiichukua jezi ya Kibu Danis baada ya mechi yoyote ukaikamua utapata jasho jingi kuliko mchezaji mwingine yeyote.

Huyu ni Simba haswaa. Hachoki na Wala hakati tamaa. Atakuja kukupoka na atakuja tena. Anageuka mbogo au kifaru uwanjani.

Kuna wakati timu inashinda mechi sio Kwa sababu ina wachezaji bora sana au Wana vipaji vya kutisha. Kuna wakati unahitaji wachezaji wapambanaji walio tayari kuvuja jasho jingi Ili kuipigania klabu.

Kama una timu ina vipaji lakini wachezaji wanasubiri mipira iwafikie miguuni na hawapo tayari kukimbia kilometa nyingi uwanjani kuwapora wapinzani mipira na mipira ya kugombea 50 Kwa 50 hawawezi kuishinda na kuwaachia wapinzani wanaishinda na kuanzisha mipango yao kwenye mfumo wao wakiwa huru huwezi kushinda mechi ya mpira wa miguu.

Kuna wakati lazima wachezaji wajitolee haswa Ili kuwanyima wapinzani kucheza wakiwa huru.

Moyo wa kujitolea na kuvuja jasho jingi mno ni kanuni namba moja ya timu inayotaka kushinda mechi ya mpira wa miguu.

Kibu Danis Prosper ni mfano hai wa wachezaji wenye moyo wa upambanaji uwanjani.

Wachezaji wote wazawa nchini Wana kitu Cha kuiga kutoka Kwa huyu mwamba.

( Jicho la tatu la Mgalilaya).

SOMA NA HII  WATANO WA SIMBA KUIKOSA KAGERA SUGAR KWA MKAPA