Home Habari za michezo ONANA AJICHIMBIA KABURI MWENYEWE MSIMBAZI

ONANA AJICHIMBIA KABURI MWENYEWE MSIMBAZI

Habari za Simba leo

Pale Simba Onana ameanza kujichimbia kaburi yeye mwenyewe kwasababu amesahau kabisa kuwa Simba sio Ihefu.

Onana hakumbuki kabisa alisajiliwa kwa gharama kubwa na mbwembwe na sasa kiwango chake kimekuwa chini sana mithili ya mizizi.Onana hawajibiki kabisa na harakati za kutaka kugusa nyota, yuko ndotoni amelala usingizi mtamu.

Bila kukupesa macho kwasasa Onana amekuwa mchezaji wa kawaida hajafikia walau tone la maji ya bahari ya utukufu wake,Onana kiwango chake kimekuwa mithili ya mayai viza,kiwango chake ni donda ndugu kwa mashabiki hakika nakwambia yuko mbali sana na matarajio.

Onana kama hatokuwa karibu na kivuli cha Kibu Denis nakwambia lazima safari ya begi kubwa itamkuta.

Onana anafikiri kucheza Simba ukiwa na kiwango cha kawaida ni jambo linalowezekana,Simba ina malengo makubwa sana kila mchezaji anayepata nafasi ya kucheza ni lazima amwage jasho mara mbili zaidi ,Simba sio sehemu ya kumpa mchezaji muda ,Simba sio udongo unaosubiri mbegu itakayokuwa matunda siku moja.Onana ukishindwa Utaondoka.

SOMA NA HII  PAMOJA NA SIMBA KUFUNGWA NA YANGA JUZI...AHMED ALLY AIBUKA NA KUJISIFU WALIVYOJAZA UWANJA .."TUMEYAONA MACHOZI"...