Home Habari za michezo KUELEKEA MECHI NA RUVU SHOOTING….AHMED ALLY AMPIGA KIJEMBE MASAU BWIRE…

KUELEKEA MECHI NA RUVU SHOOTING….AHMED ALLY AMPIGA KIJEMBE MASAU BWIRE…


Mabingwa wa Soka Tanzania Bara Simba SC wameipiga kijembe Ruvu Shooting kuelekea mchezo wa Mzunguuko wa 23 wa Ligi kuu, utakaozikutanisha timu hizo keshokutwa Jumapili (Mei 08), Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam.

Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Simba SC Ahmed Ally amesema kikosi chao kipo tayari kwa mchezo huo, na wana imani kitapambana vilivyo ili kuvuna alama tatu muhimu.

Amesema Ruvu Shooting mara zote inapokutana na Simba SC hutangaza vita, lakini hushindwa kupigana vita na kujikuta mwisho wa dakika 90 inakubali kuachia alama tatu.

“Kuna kutangaza vita na kuna kupigana vita, Ruvu Shooting miaka yao yote huwa wanatangaza vita lakini huwa hawapigani vita ndio maana wapo kwenye nafasi ya kushuka daraja” Ahmed Ally

Mara ya mwisho timu hizo zilipokutana Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza Ruvu Shooting iliyokua mwenyeji ilikubali kufungwa mabao 3-1.

SOMA NA HII  KUELEKEA MECHI NA SIMBA KESHO....MABOSI AZAM FC WAAMUA KUFANYA UAMUZI HUU MGUMU....

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here