Home Habari za michezo GAMONDI ATUMIA DAKIKA 180 KUWASOMA SIMBA

GAMONDI ATUMIA DAKIKA 180 KUWASOMA SIMBA

Ni Miguel Gamondi, Kocha Mkuu wa Yanga amewasoma wapinzani wao Simba kwa muda wa dakika 180 baada ya kuwachambua wapinzani wake.Novemba 5 Yanga wanatarajiwa kuwa wageni wa Simba kwenye mchezo wa Kariakoo Dabi, Uwanja wa Mkapa.

Yanga imekusanya pointi 18 baada ya kucheza mechi saba huku Simba pia wakiwa na pointi 18 baada ya kucheza michezo sita.

Gamondi alitumia dakika 90 za kwanza za mchezo wa robo fainali ya AFL ambapo alitua kwa Mkapa kutazama mchezo huo ambao ulimalizika kwa Simba kutoa sare ya mabao 2-2.

Mchezo mwingine ambao Gamondi aliweza kuushuhudia ulikuwa ni ule wa dhidi ya Ihefu wa ligi kuu ambapo Simba waliibuka na ushindi wa mabao 2-1.

Kocha Gamondi atakuwa na kazi moja tu ya kuhakikisha kuwa anaipa ushindi yanga mara baada ya msimu uliopita Yanga kupoteza kwa idadi ya mabao 2-0 dhidi ya Simba kocha akiwa ni Nassredine Nabi.

Ahmed Ally, Meneja wa Idara ya Simba amesema kuwa wanatambua kwamba kocha wa Yanga alikuwa akiwafuatilia hivyo hawana mashaka.

SOMA NA HII  AZAM FC WAGOMEA MAKOCHA WABONGO...IBENGE KUMWAGA WINO