Home CAF AS VITA YAIPIGA MKWARA SIMBA, YAZITAKA POINTI TATU KWA MKAPA

AS VITA YAIPIGA MKWARA SIMBA, YAZITAKA POINTI TATU KWA MKAPA


FLORENT Ibenge, Kocha Mkuu wa timu ya AS Vita ya DR Congo amesema kuwa watapambana kupata ushindi mbele ya Simba kwenye mchezo wao wa Ligi ya Mabingwa Afrika unaotarajiwa kuchezwa Aprili 3, Uwanja wa Mkapa.

Kocha huyo amesema kuwa wanatambua mchezo huo utakuwa na ushindani mkubwa ila hakuna namna lazima wapate ushindi.

Ndani ya Ligi ya Mabingwa Afrika, AS Vita imekusanya pointi nne baada ya kushinda mchezo mmoja dhidi ya Al Merrikh ugenini kwa ushindi wa mabao 4-1 na ililazimisha sare ya kufungana mabao 2-2 dhidi ya Al Ahly ikiwa ugenini ila ilipoteza kwa kufungwa mabao 3-0 ikiwa nyumbani.

Rekodi zinaonyesha kuwa AS Vita wamekuwa imara msimu huu wakiwa ugenini ila wakiwa nyumbani wanapoteza kwani hata Simba ilishinda bao 1-0 kwenye mchezo wa kwanza hatua ya makundi walipowafuata.

AS Vita inahitaji pointi tatu kama ambavyo Simba inayonolewa na Didier Gomes inazihitaji jambo ambalo linaongeza ushindani kwenye mchezo huo, Uwanja wa Mkapa.

Ibenge amesema:”Tuna mchezo mgumu na mzuri kwa sababu wapinzani wangu ninawatambua namna wanavyohitaji ushindi na wakiwa nyumbani vile wanacheza.

“Hakuna namna tunahitaji kusonga mbele na njia pekee ya kuweza kusonga mbele ni kushinda mechi zetu ikiwa ni pamoja na ile dhidi ya Simba,” .

Kwenye kundi A, Simba inaongoza ikiwa na pointi 10 inahitaji pointi moja kutinga hatua ya robo fainali na AS Vita ipo nafasi ya tatu na pointi nne inahitaji pointi tatu kufufua matumaini ya kutinga hatua ya robo fainali kwa sababu nafasi ya pili ipo mikononi mwa Al Ahly wenye pointi 7 ambazo zinaweza kufikiwa nao.

Hesabu kwa AS Vita akishinda mechi zake zote mbili atafikisha pointi 10 ambazo Simba anazo kwa sasa hivyo ili kuweza kutinga hatua ya robo fainali ni lazima shinde mechi zote kwa idadi ya mabao mengi huku akisubiri matokeo ya wapinzani wake.

Kundi A limekuwa na ushindani mkubwa ambapo ikiwa Simba akipoteza mechi zake mbili zijazo anaweza kushushwa nafasi hiyo na kuibukia nafasi ya tatu hivyo ili aweze kujihakikishia nafasi ya kutinga hatua ya robo fainali ni lazima ashinde mbele ya AS Vita ama alazimishe sare na kusepa na pointi moja itakayomfanya afikishe pointi 11.

SOMA NA HII  SIMBA ,YANGA,AZAM NA BIASHARA KUJUA WAPINZANI WAO CAF LEO