Home Habari za michezo SIRI IMEVUJA YANGA WAMUAGA RASMI MAYELE, MAMBO YAPO HIVI

SIRI IMEVUJA YANGA WAMUAGA RASMI MAYELE, MAMBO YAPO HIVI

NYOTA YA MAYELE YAZIDI KUWAKA...AFANYA MAKUBWA HAYA MAPYA

Baada ya kukaa Yanga kwa misimu miwili, sasa ni rasmi, Fiston Mayele anaondoka nchini kwenda kujiunga na timu yake mpya, Uarabuni, wikiendi hii, huku Pyramid ya misri ikitajwa.

Licha ya Yanga na Mayele kufanya siri, lakini Mwanaspoti limepenyezewa na moja ya vigogo wa juu wa timu hiyo, tayari Yanga imeingiziwa fedha zake za mauzo ya Mayele ambazo ni zaidi ya Sh2 bilioni na nyota huyo ataondoka nchini muda wowote kuanzia leo.

Tayari Mayele amewaaga wachezaji wenzake na viongozi wa Yanga na juzi alipiga picha na kurekodi video ambazo Yanga itazichapisha kwenye mitandao yao ya kijamii muda wowote zikiwa na maudhui ya kuaga.

chanzo chetu kimeenda mbali na kuwatafuta viongozi wa juu wa Pyramids inayohusishwa na kumnunua Mayele na kuthibitisha kuwapo kwa mazungumzo baina yao na nyota huyo raia wa DR Congo.

“Ndiyo, mazungumzo kati yetu na Myele yapo na sasa yemefika katika hatua za mwisho,” alisema Omar el Feky, mmoja ya viongozi wa timu hiyo.

Mayele atakumbukwa Yanga kwa ubora wake wa kupachika mabao na katika misimu miwili aliyokaa Jangwani amecheka na nyavu mara 33 kwenye Ligi Kuu katika misimu yake miwili.

Alianza na mabao 16 msimu wa kwanza na kukikosa kiatu cha dhahabu kilichokwenda kwa George Mpole aliyekuwa Geita Gold na kufunga mabao 17 na katika msimu wa pili alitupia mipira 17 nyavuni na kumaliza kinara akilingana na Saido Ntibazonkiza wa Simba.

Msimu uliopita, alifunga mabao mengine 14 katika mashindano ya CAF. Alifunga kwanza mara saba katika mechi za awali za Ligi ya Mabingwa, kisha mengine saba katika Kombe la Shirikisho Afrika na Yanga ilifika fainali na kuzidiwa na USM Alger ya Algeria iliyotwaa ubingwa kwa faida ya bao la ugenini baada ya sare ya 2-2.

Mabao hayo ni tofauti na yale aliyofunga katika mashindano ya Kombe la FA (ASFC) na Ngao ya Jamii.

SOMA NA HII  CHAMA HALI SI HALI SIMBA MAMBO YAZIDI KUWA MAGUMU