Home EURO 2020 DAEI AMPONGEZA RONALDO KWA KUFIKIA REKODI YAKE YA MABAO 109

DAEI AMPONGEZA RONALDO KWA KUFIKIA REKODI YAKE YA MABAO 109


MSHAMBULIAJI wa zamani wa timu ya Taifa ya Irani, Ali Daei amempongeza mshambuliaji na nahodha wa timu ya taifa ya Ureno, Cristiamo Ronaldo kufuatia nyota huyo kufikia rekodi ya mabao 109 katika michezo ya kimataifa.

Ronaldo alifikia rekodi hiyo baada ya kufunga mabao mawili kwa mikwaju ya penalti katika mchezo wao wa jana dhidi ya Ufaransa.

Daei aliwasilisha pongezi hizo kupitia mtandao wake wa kijamii wa Instagram ambapo ameandika: “Hongera sana Cristiano ambaye sasa umebakiza bao moja kuvunja rekodi ya kufunga mabao kwa wanaume kimataifa.

“Ni heshima kubwa kwamba mafanikio haya kwa sasa yatakuwa ya Ronaldo bingwa mkubwa wa soka, na binadamu anayejali ambaye pia huchochea huwapa moyo wengine.”

SOMA NA HII  URENO YATINGA 16 BORA, RONALDO NA MSHIKAJI WAKE BENZEMA WAKIWASHA