Home Uncategorized NAMNA SERIKALI ILIVYOMRUDISHA MO DEWJI SIMBA

NAMNA SERIKALI ILIVYOMRUDISHA MO DEWJI SIMBA


Baada ya Mwekezaji Mkuu wa klabu ya Simba, Mo Dewji kutangaza kujiondoa katika Bodi ya klabu hiyo, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ambaye pia ni shabiki mkubwa wa Simba SC, usiku wa kuamkia jana ametumia ukurasa wake wa insta kuwaomba mashabiki wa klabu hiyo watulie, kuhusiana na taarifa ya twitter ya mwenyeki wao wa bodi MO Dewji kutangaza kujiuzulu nafasi yake Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa klabu hiyo, kutokana na Simba kufungwa katika mchezo wa fainali ya Kombe la Mapinduzi 2020 kwa goli 1-0 dhidi ya Mtibwa Sugar.
Makonda ambaye ni kiongozi nayeiwakilisha serikali katika mkoa wa Dar es Salaam, aliandika hivi:-

“Matokea ya Mpira huleta furaha na huzuni kwa wanaofungwa. Natoa pole Kwa team yangu ya Simba pamoja na Mashabiki wote na wanaoitakia mema SIMBA. Sina uhakika na kinachoendelea kwenye Ac ya MO kama ni @moodewji mwenyewe ameandika. Nawaomba wanasimba tutulie tutapata ukweli muda si mrefu. Tusisahau kuwa Wapo watu pia wabaya hutumia mwanya huu kuvuruga Amani na utulivu wa Team zetu. Simba nguvu moja.” alisema RC Makonda
SOMA NA HII  HATMA YA CIOABA NDANI YA AZAM FC IPO NAMNA HII