WAKATI Yanga ikiendelea kufanya usajili wake, mabosi wa Simba nao tayari wameanza mambo kimyakimya kukisuka upya kikosi chao.
Mpaka sasa Simba, inaelezwa kuwa tayari imefanikiwa kumalizana na mshambuliaji wa Yanga, Ibrahimu Ajibu ambaye amesaini mkataba wa miaka miwili wa kuitumikia timu hiyo, lakini pia ipo katika hatua za mwisho za kumalizana na kiungo mshambuliaji wa Gor Mahia pamoja na timu ya taifa ya Kenya, Francis Kahata pamoja na beki wa kulia wa Lipuli FC, Haruna Shamte.
Habari za kuaminika kutoka ndani ya Simba, ambazo Championi Ijumaa limezipata zimedai kuwa Ajibu tayari ameshamalizana na uongozi huo ambapo usajili wake pamoja na mshahara umegharimu timu hiyo Sh milioni 258 katika muda wote wa mkataba wake.
Inadaiwa kuwa fedha ya usajili pekee ambayo amepewa ni Sh 90m huku mshahara ambao atakuwa akilipwa kwa mwezi ni Sh 7m, hivyo kwa kipindi chote cha miaka miwili atakayokuwa na Simba jumla ya mshahara wake utakuwa ni Sh 168 milioni.
“Kwa hiyo ukizijumlisha fedha hizo za mshahara ambazo atalipwa kwa miaka hiyo miwili pamoja na zile za usajili utangundua kuwa jumla ya fedha atakazochukua akiwa Simba ni Sh 258m.
“Hata hivyo mpaka sasa ameshalipwa Sh 80m, ambapo tayari ameshaanza kuzifanyia kazi kwa kumalizia ujenzi wa nyumba yake kwa kuiwekea marumaru ‘tiles’ pamoja na madirisha ya vioo,” kilisema chanzo hicho cha habari.
Ishu ya Kahata “Uongozi wa Simba upo katika hatua za mwisho kwa ajili ya kumalizana naye na umepanga kumsainisha mkataba mapema kabla ya kuanza majukumu ya kuitumikia timu yake ya taifa ya Kenya kwenye
Kombe la Mataifa Afrika (Afcon) baadaye mwezi ujao huko nchini Misri,” kilisema chanzo. Alipotafutwa Kahata mwenyewe alisema: “Ishu hiyo bado haijakamilika, nipo nyumbani Kenya nikiwa na timu ya taifa, tunajiandaa na Afcon ambapo kesho (leo) Ijumaa tunasafiri kuelekea Ufaransa kuweka kambi.”
Simba wanamtaka Kahata kuchukua nafasi ya Mganda Emmanuel Okwi ambaye anatarajia kuondoka ndani ya kikosi hicho. Shamte Haruna Shamte wa
Lipuli FC yeye tayari ameshamalizana na klabu hiyo kwenye mazungumzo ambapo imebaki suala la kusaini mkataba tu. “Analetwa maalum kwa ajili ya kuchukua nafasi ya Zana Coulibaly ambaye ana uwezekano wa kuachwa pamoja na Shomari Kapombe ambaye amekuwa na majeraha ya mara kwa mara,” kilisema chanzo.
Inaelezwa kuwa Kocha wa Simba, Patrick Aussems anahitaji kusajili beki wa kati, beki wa kushoto, kiungo mkabaji pamoja na mshambuliaji
Home Uncategorized SIMBA YAZIDI KUJIBU MAPIGO JANGWANI, KAHATA, SHAMTE NI MUDA WOWOTE, YUPO MMOJA...