Home Habari za michezo BANGALA ATOBOA SIRI NZITO ZA YANGA…WANATUMIA UCHAWI HUU KUPATA MATOKEO

BANGALA ATOBOA SIRI NZITO ZA YANGA…WANATUMIA UCHAWI HUU KUPATA MATOKEO

KIUNGO MGANDA AWACHANA MUDAHTIR NA BANGALA...AWATOBOLEA SIRI MECHI NA MAZAMBE

Kiungo wa Young Africans, Yannick Bangala Litombo ameutaja Uchawi wa klabu hiyo ambao umewafanya kuwika katika michuano ya kimataifa safari hii huku akiweka wazi kuwa mshikamano uliopo baina ya wachezaji, benchi la ufundi na viongozi ndio sababu kubwa.

Young Africans wamefuzu katika hatua ya Robo Fainali ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika kwa mara ya kwanza mara baada ya kukaa kwa zaidi ya miaka 15 bila kufika katika hatua hiyo jambo ambalo ni la kujivunia kwa timu hiyo.

“Mchawi wetu ndani ya Young Africans ni sisi wenyewe wachezaji, bechi la ufundi na viongozi kwa pamoja ambalo tunaendelea kufanya kazi yetu vyema na kwa malengo makubwa.”

“Kwa pamoja tumekuwa tukizungumza mara kwa mara kuhusiana na kupata mafanikio kutokana na melngo ambayo tulijiwekea na ndio maana unao kama kila kitu kimewezekana, tumeongoza kundi lakini tunaongoza na ligi kuu kwa ujumla.”

“Kwa sasa tunaangalia nini tukifikie huko mbeleni na hiyo inabaki kuwa ni siri kati ya wachezaji benchi la ufundi na viongozi, kwa upande wa mashabiki tunaendelea kuwashukuru kwani wamekuwa sehemu ya kuirudisha heshima timu katika michuano ya kimataifa mara baada ya kushindwa kufanya hivyo kwa muda mrefu,” amesema mchezaji huyo

SOMA NA HII  YANGA YATOA TAMKO KUHUSU CEDRIC KAZE