Home Uncategorized OKWI NA SIMBA WATUNISHIANA MISULI, TIMU ILIYO KARIBU KUMALIZANA NAYE YATAJWA

OKWI NA SIMBA WATUNISHIANA MISULI, TIMU ILIYO KARIBU KUMALIZANA NAYE YATAJWA


Mitandao na Magazeti ya kuaminika ya Afrika Kusini yamesema uwezekano wa Emmanuel Okwi kusaini Kaizer Chiefs ni asilimia 85, lakini Simba wamedai haendi kokote.

Okwi mwenyewe ameiambia televisheni ya Afrika Kusini ya SABC kwamba anaweza kucheza Sauzi au nje ya hapo lakini ataamua baada ya Afcon kumalizika.

Habari zinasema kwamba Kaizer ambayo tayari imemsainisha kiungo wa Simba, James Kotei imepania kumshusha Okwi na inadaiwa tayari ameshasaini mkataba wa awali lakini anawazuga Simba.

Simba na Okwi kwa sasa wanavutana juu ya mkataba mpya ambapo Mganda huyo anasitasita kusaini mkataba mpya baada ya ule wa awali wa miaka miwili kumalizika.

Mtendaji mkuu wa Simba, Crescentius Magori ameliambia Championi Jumatano, kuwa wana matumaini ya kumbakisha Okwi kutokana na kufikia sehemu nzuri ya mazungumzo.

“Hilo suala tunazungumza hadi sasa na uzuri ni kwamba anaweza kubakia kwa msimu ujao kwani tupo sehemu nzuri ya mazungumzo.

“Imani yetu ni kwamba Okwi tutakuwa naye, kwani anaelekea kukubaliana na kile ambacho sisi tumemwambia ili awepo kikosini kwa msimu ujao,” alisema Magori ambaye ni msomi. Kwa misimu miwili ambayo Okwi amekaa ndani ya Simba amefanikiwa kufunga mabao 34 katika Ligi Kuu Bara.

SOMA NA HII  LIVERPOOL INA KAZI KWELI KESHO MBELE YA TOTTENHAM