Home news FEISAL SALUM ATEMBEZA BONGE MOJA YA MKWARA

FEISAL SALUM ATEMBEZA BONGE MOJA YA MKWARA


FEISAL
 Salum ‘Fei Toto’, amesema hawatakuwa tayari kuona wanapoteza mchezo wowote katika ligi misimu huu, ukiwemo dhidi ya Simba, kwa kuwa anaamini wana kikosi bora tofauti na wapinzani wao.


Kiungo huyo ametoa kauli hiyo kufuatia kufanikiwa kufunga bao pekee katika mchezo wa kwanza wa Ligi Kuu Bara uliopigwa Uwanja wa Kaitaba mkoani Kagera na Yanga iliibuka na ushindi wa bao 1-0.

Mfungaji wa bao la kwanza kwa Yanga ni Fei ambaye aliweza kuipa pointi tatu timu hiyo inayonolewa na Kocha Mkuu, Nasreddine Nabi.

Akizungumza na Championi Ijumaa, Fei Toto alisema kuwa imekuwa ni furaha kubwa kwake kufunga bao la kwanza katika msimu huu kwa timu yake, hali ambayo anaamini itaongeza hali ya kupambana kwa timu nzima kwa kuwa hawatakuwa tayari kupoteza mchezo wowote msimu huu.


“Kwanza, kwangu imekuwa furaha ya kuweza kufunga bao la kwanza kwa timu yangu msimu huu, hii ni hatua nzuri kwa sababu tupo hapa kwa ajili ya kufikisha malengo ya timu kuona tunapata matokeo katika kila mchezo.


“Ligi ni ngumu kwa kuwa kila timu imejiandaa kupata matokeo.Wapinzani wetu nao wanahitaji matokeo mazuri lakini bahati imekuwa upande wetu tumeshinda maana naamini hatutakuwa tayari kuona tunapoteza mchezo wowote msimu huu ili kuweza kufikia malengo,” alisema Fei Toto.

Mchezo wa pili wa Yanga ilishinda kwa bao 1-0 dhidi ya Geita Gold na kuweza kufikisha jumla ya pointi sita kibindoni.


SOMA NA HII  AZAM: 'UNBEATEN' YA YANGA ILILINDWA SANA NA WAAMUZI...