Home news MAJEMBE MAPYA YANGA YAWEKA REKODI YAO

MAJEMBE MAPYA YANGA YAWEKA REKODI YAO


 YANGA imeweka rekodi nzuri katika msimu 
huu ya kuanza msimu mpya wa Ligi Kuu Bara kwa ushindi wa bao 1-0 tofauti na misimu miwili mfululizo ambapo hawakuweza kupata ushindi.

Na kwenye mchezo wao wa pili wa ligi walishinda kwa bao 1-0 dhidi ya Geita Gold katika mchezo wa kwanza uliochezwa Uwanja wa Mkapa.

Timu hiyo imepata ushindi huo baada ya kuwafunga Kagera Sugar katika mchezo wa ligi uliochezwa Uwanja wa Kaitaba,Bukoba.

Rekodi hiyo imenogeshwa na wachezaji wapya ambao wamesajiliwa na timu hiyo katika msimu huu baadhi ni Fiston Mayele, Yannick Bangala,Djigui Diarra, Heritier Makambo, Shaban Djuma na Jesus Moloko.

Ushindi huo unaifanya Yanga kuweka rekodi baada ya misimu miwili mfululizo kushindwa kuanza na ushindi.

Msimu uliopita 2020/2021 ilianza kwa sare ya bao 1-1 dhidi ya Tanzania Prisons na 2019/2020 ilifungwa nyumbani na Ruvu Shooting bao 1-0.

Yanga imeendelea kuwapa raha wadau na mashabiki wake baada ya kuibuka na ushindi katika mchezo dhidi ya Kagera Sugar bao 1-0 kwenye Uwanja wa Kaitaba.

Katika mchezo huo, aliyepeleka furaha kwa Wanayanga ni kiungo Feisal Salum ‘Fei Toto’ dakika ya 24.


Akizungumzia hilo, Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano wa Yanga, Hassani Bumbuli alisema: “Ni furaha kubwa kwa mashabiki wetu kuwaona wakiendelea kupata furaha na burudani.

“Hiyo ni ishara tosha kuamini kuwa viongozi na benchi la ufundi limefanya usajili bora katika msimu huu na kikubwa ni kuchukua makombe yote tutakayoyashindania katika msimu.

“Tuendelee kuwaunga mkono wachezaji na benchi la ufundi kwa kujitokeza uwanjani kwa ajili ya kuwasapoti wanapoipambania timu yao ya Yanga.”


SOMA NA HII  ONYO HILI LAMFUATA LOMALISA HUKOHUKO NJE YA UWANJA