Home news SIMBA YABAINISHA KILICHOWAFANYA WAKAANZA KWA KUSUASUA

SIMBA YABAINISHA KILICHOWAFANYA WAKAANZA KWA KUSUASUA


 DIDIER Gomes, Kocha Mkuu wa Simba amesema kuwa walianza kwa kusuasua kwenye Ligi Kuu Bara kwa kuwa walikuwa bado hawajajua ligi itakuwa ya aina gani kwa msimu wa 2021/22.

Tayari mabingwa hao watetezi wa taji la Ligi Kuu Bara wameambulia ushindi mmoja kwenye mchezo wa ligi na walitoshana nguvu na Biashara United kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara uliochezwa Uwanja wa Karume, Mara.

Gomes amebainisha kwamba kwenye mchezo wa kwanza walipata shida kuweza kushinda kwa kuwa walikuwa bado hawajajua aina ya ligi itakavyokwenda.

“Tulianza kwa shida msimu huu kwa kuwa hatukujua ligi inakwendaje na hilo limetufanya tuweze kujua namna gani tunaweza kwenda hiloawali lilitufanya tukashindwa kupata ushindi mchezo wetu wa kwanza mbele ya Biashara United.

“Kwa sasa tumejua aina ya ligi ilivyo na mtindo ambao unahitajika tutakwenda sawa na imani yetu ni kuona kwamba tunapata matokeo chanya kwenye mechi zetu ambazo tutacheza,” amesema.

Katika mchezo wa kwanza kushinda ilikuwa ni mbele ya Dodoma Jiji na ilishinda kwa bao 1-0 dhidi ya Dodoma Jiji katika mchezo uliochezwa Uwanja wa Jamhuri,Dodoma.

SOMA NA HII  SIMBA YATUA MOROCCO KISHUJAA...KINA TUISILA WADUWAA..ADEBAYOR KUJA SIMBA NI MUDA TU...