Home Uncategorized ISHU YA BILIONI 20 YA MO YAMUIBUA MWENYEKITI ATOA NENO HILI

ISHU YA BILIONI 20 YA MO YAMUIBUA MWENYEKITI ATOA NENO HILI


ALIYEWAHI kuwa Mwenyekiti wa Klabu ya Simba, Swedy Mkwabi ameitaka Bodi ya Wakurugenzi ya klabu hiyo kushughulikia masuala yote ya muhimu ikiwemo kuhakikisha Sh. bilioni 20 zinawekwa kwenye akaunti.
Mkwabi amesema Simba ndani ya uwanja haina shida kwa kuwa inakwenda vizuri, kilichobaki ni kwa bodi inayoongozwa na Mohammed Dewji ‘Mo’ ishughulikie mambo ya nje ya uwanja ambayo yataonekana na mashabiki.
Mkwabi aliwahi kuwa mwenyekiti wa klabu hiyo, aliyepata nafasi ya kuiongoza Simba kwa muda mfupi, kisha baadaye akaamua kujiondoa kwenye nafasi hiyo kwa kile kilichodaiwa kuwa na mgogoro wa chini kwa chini na Mo.

Akizungumzia ishu hiyo, Mkwabi alisema ipo haja ya Bodi ya Wakurugenzi ya Simba kushughulikia masuala ambayo yapo nje ya uwanja yanayoonekana kwa mashabikina wanachama,huku akisisitiza kuwa moja ya vitu vya msingi ni kuhakikisha ile Sh bilioni 20 aliyoahidi Mo inawekwa kwenye akaunti kama ambavyo mwekezaji huyo aliahidi.

“Simba haina shida ndani ya uwanja, kama matokeo inapata na ina wachezaji wazuri, kwa sasa sipo kwenye uongozi wa klabu hiyo, lakini nazungumza kama mwanachama na Mwanasimba, niiombe Bodi ya Wakurugenzi kuhakikisha inashughulikia masuala mbalimbali yatakayojenga klabu nje ya uwanja, ikiwemo Sh bilioni 20 kuwekwa kwenye akaunti ya klabu kama ambavyo Mo aliahidi wakati anataka uwekezaji,” alisema Mkwabi.
Suala hilo la Sh bilioni 20, liliungwa mkono na Mwenyekiti wa zamani wa klabu hiyo, Ismail Aden Rage ambaye naye alipoulizwa alisema: “Kama kweli Mo hajaweka hizo katika Fixed Account ya klabu atakuwa anafanya makosa, kwa sababu ni kitu ambacho aliahidi na Wanasimba wanatakiwa kuona hilo linatekelezwa, watu wa Simba pia hamtakiwi kukaa kimya, semeni ukweli kama mnaona mambo hayaendi vizuri.”
Kaimu Mwenyekiti wa Simba, Mwina Kaduguda ili azungumzie ishu hiyo ya Sh bilioni 20, ambapo alijibu kuwa: “Hayo mambo wala sisi hayatusumbui, tunachoangalia ni kufikia malengo na kuyafikia mabadiliko ya kiuendeshaji, kuhusu Sh bilioni 20, kwa kifupi tu zilishawekwa kwenye akaunti na bado hazijaanza kutumika kabisa.”

Chanzo Championi
SOMA NA HII  MTIBWA SUGAR: TUPO TAYARI KWA AJILI YA KUENDELEA KUPAMBANA