Home Uncategorized SIMBA YAPANIA KUMCHOMOA BEKI MMOJA POLISI TANZANIA

SIMBA YAPANIA KUMCHOMOA BEKI MMOJA POLISI TANZANIA


IMEELEZWA kuwa uongozi wa Simba upo kwenye hesabu za kuinasa saini ya beki mpambanaji ndani ya Polisi Tanzania, Idd Mobby.

Mobby ambaye ni nahodha pia wa Polisi Tanzania amewakuwa kwenye ubora wake msimu huu jambo lililowavutia mabosi wa Simba ambao wanapanga kuboresha kikosi chao kwa sasa.
Nyota huyo mzawa amewahi kukipiga pia ndani ya Toto Africans na Mwadui FC.
Ofisa Habari wa Polisi Tanzania, Frank Lukwaro amesema kuwa kwa sasa hawajapata taarifa yoyote kuhusu Mobby hivyo hawezi kuzungumza jambo.
SOMA NA HII  AZAM FC YAANZA KUIWINDA SIMBA, YAPANIA KUFANYA MAAJABU