Home Uncategorized KAZI IMEANZA, AZAM FC SASA KUSHUSHA MASHINE ZA KAZI NNE

KAZI IMEANZA, AZAM FC SASA KUSHUSHA MASHINE ZA KAZI NNE


UONGOZI wa Azam FC umeamua kuweka wazi dhamira yao ya kutaka kushindana na klabu kongwe katika Ligi Kuu Bara, Simba na Yanga katika masuala ya usajili wa wachezaji watakaokiimarisha kikosi chao kwa ajili ya kupindua utawala wa timu hizo.
Awali Azam FC waliweza kupindua utawala wa timu hizo msimu wa 2013/2014 baada ya kufanikiwa kutwaa ubingwa wa ligi kuu kwa mara ya kwanza tangu ilipopanda kwa kufikisha pointi 59 ikiwa na mchezo mmoja mkononi, ambazo zilikuwa haziwezi kufikiwa na timu yoyote.
Imeelezwa kuwa uongozi wa timu hiyo umepanga kuwapiga chini baadhi ya nyota wake mwishoni mwa msimu huu baada ya kushindwa kuonyesha viwango bora huku wakipania kuwanasa nyota wengine kutoka nje.
Ofisa Habari na Mawasiliano wa Azam FC, Zakaria Thabit amesema:-“Ni kweli tuna mipango ya kufanya usajili, kwa sababu sisi ni timu kubwa na sifa ya timu kubwa yoyote duniani ni lazima ifanye usajili, kwa hiyo hata sisi tunataka kusajili wachezaji wengine wanne kutoka nje ili tuboreshe kikosi chetu, tunataka kipa, beki, kiungo na mshambuliaji.
“Hatufanyi hivi kwa kuwa tuna pengo sehemu yoyote ila ni kwa ajili ya kuwatengenezea changamoto na bidii wachezaji wetu,” alisema Zakaria.

SOMA NA HII  KIMENUKA!! MCHEZAJI YANGA AAMUA KUKIWASHA, AMKATAA KOCHA MPYA