Home Habari za michezo HIVI NDIVYO NBC PREMIER LEAGUE ILIVYOMALIZIKA KWA REKODI ZA KIBABE…

HIVI NDIVYO NBC PREMIER LEAGUE ILIVYOMALIZIKA KWA REKODI ZA KIBABE…


Hatimaye Klabu ya Yanga imefanikiwa kutwaa Ubingwa wa Ligi Kuu ya NBC bila kupoteza mchezo wowote baada ya kuibuka na ushindi wa bao moja kwa bila dhidi ya Mtibwa Sugar bao lililowekwa kimiani na Denis Nkane katika dakika ya 80.

Kwa matokeo hayo Yanga imemaliza msimu ikiwa na jumla ya alama 72 huku ikiwa na wastani wa magoli 40 ya kufunga na kufungwa.

Baada ya mchezo huo Yanga itajiandaa kuelekea Jijini Arusha ambapo itakwenda kucheza dhidi ya Coastal Union katika mchezo wa Fainali ya Kombe la Shirikisho la Azam Sports.

Kwa upande mwingine klabu ya Biashara United imeungana na Mbeya Kwanza kwa timu zilizoshuka daraja huku Tanzania Prisons na Mtibwa Sugar zikinusurika kushuka na hivyo zitajiandaa kucheza Play-Off.

Aidha mshambuliaji wa Geita Gold FC George Mpole ameibuka mfungaji Bora wa Ligi Kuu ya NBC msimu huu akiwa na jumla ya mabao 17 na pasi 4 za mabao huku akifuatiwa na mshambuliaji wa Yanga Fiston Mayele aliyemaliza msimu akiwa na mabao 16 na pasi 5 za mabao.

SOMA NA HII  RASMI....HATIMAYE KELVIN JOHN AWEKA REKODI NYINGINE ULAYA...ACHUKUA NAFASI YA MJAPANI...