Home Habari za michezo PAMOJA NA KUTOCHEZA MECHI NYINGI MSIMU HUU…”NINJA” AINAMISHA KICHWA CHINI NA KUFUNGUKA...

PAMOJA NA KUTOCHEZA MECHI NYINGI MSIMU HUU…”NINJA” AINAMISHA KICHWA CHINI NA KUFUNGUKA HAYA KWA YANGA…


Beki wa Yanga, Abdallah Shaibu ‘Ninja’ amesema japokuwa amekaa nje muda mrefu bila kucheza msimu huu, kitendo cha kuvaa medali ya ubingwa kimeondoa machungu ya majeraha aliyokuwa anayapitia.

Kwa mara ya kwanza Ninja alijiunga Yanga msimu wa 2017-2019, hakuwahi kuchukua ubingwa, baada ya kufanikiwa msimu huu hakusita kuelezea furaha yake ya kuwa miongoni mwa wachezaji watakaoandikwa kwenye vitabu vya kumbukumbu vya klabu hiyo.

“Ubingwa ni raha jamani, najisikia raha iliyopitiliza kuvaa medali msimu huu, pia ni spesho kwa mke wangu maana nilikuwa naye muda mrefu lakini baada ya kufunga ndoa Yanga inachukua ubingwa,” alisema Ninja na kuongeza;

“Nawashukuru mashabiki waliotuvumilia kipindi kirefu na timu haikuchukua ubingwa, niwaambie kwamba kwa sasa nipo fiti kufanya kazi msimu ujao,”.

Ninja alisema Yanga ina baraka nyingi katika maisha yake ya soka, kwani kupitia timu hiyo ndio sababu ya kupata ofa katika klabu ya MFK Vyškov ya Jamhuri ya Czech barani ulaya, 2019/20.

“Japokuwa ilinitoa kwa mkopo kwenda kucheza LA Galaxy II ya Marekani nisingefika huko bila kuonekana Yangan ndio maana nasema kwangu ina historia ya aina yake,” alisema.

Naye Nahodha wa zamani wa timu, Nadir Haroub ‘Cannavaro’ alisema hakumkabidhi jezi 23 Ninja kwa bahati mbaya.

“Ninja ana kipaji kikubwa sana, nadhani majeraha ndio yamemfanya asicheza kwa muda mwingi, ila naamini kabisa atafanya mambo makubwa ndani ya kikosi cha Yanga,” alisema.

SOMA NA HII  TWAHA KIDUKU: NGUMI ZANGU ZINAUMA