Home Uncategorized SIMBA YATUMA UJUMBE MZITO KWA YANGA

SIMBA YATUMA UJUMBE MZITO KWA YANGA


JOHN Bocco nahodha wa Simba amesema kuwa msimu ujao watapambana kufa na kupona kutetea taji lao na kufanya vyema michuano ya kimataifa.

Simba ni mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Bara wana kibarua kizito cha kutetea kombe hilo kutokana na mipango ya wapinzani wao Yanga kupigia hesabu ubingwa.

 Hesabu hizo ni ujumbe mzito kwa Yanga na timu nyingine zinazoshiriki ligi ambazo ni Azam FC, KMC, Namungo Fc.

“Tunajua kazi itakuwa kubwa msimu ujao ila hatujakata tamaa tunapambana hesabu zetu ni kuona tunafikia malengo yetu ya kutetea kombe letu ligi itakapoanza,” amesema Bocco.

Simba imeweka kambi nchini Afrika Kusini na Yanga imeweka kambi Morogoro kwa ajili ya maandalizi ya msimu ujao.

SOMA NA HII  MNIGERIA : HUYU NDEMLA HUYU..!!!