Home Simba SC SIMBA SC WAPEWA KAIZER CHIEFS ROBO FAINALI CAF

SIMBA SC WAPEWA KAIZER CHIEFS ROBO FAINALI CAF


KLABU ya Simba imepangwa kucheza na Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini katika hatua ya robo fainali kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika katika ratiba iliyopangwa leo jioni.

Simba watacheza mchezo wa kwanza Mei 14 nchini Afrika Kusini kisha watarudiana Tanzania Mei 21-22 mchezo utakaopigwa katika uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.

Mabingwa hao watetezi wa  ligi kuu Tanzania wameingia hatua ya robo fainali ya Mabingwa baada ya kumaliza katika nafasi ya kwanza kwenye kundi A wakiwa na pointi 13.

Simba katika mechi sita za kundi hilo walishinda nne, sare moja na kupoteza mchezo mmoja.

Mechi zingine ni Al Ahly dhidi ya Mamelod Sundowns, Mc Alger dhidi ya Wydad Club na Cr Belouizdad dhidi ya Esperance.

SOMA NA HII  NYOTA WANNE SIMBA WAWEKA REKODI BONGO