Home Habari za michezo IMEISHA HIYOOO….RUDIGER AIPIGA CHINI CHELSEA MAZIMA,..MADRID WAJIOKETEA TENA EMBE KWENYE MBUYU…

IMEISHA HIYOOO….RUDIGER AIPIGA CHINI CHELSEA MAZIMA,..MADRID WAJIOKETEA TENA EMBE KWENYE MBUYU…


Beki wa klabu ya Chelsea na timu ya taifa ya Ujerumani Antonio Rudiger amekubali kujiunga na klabu ya Real Madrid mara baada ya kutosaini Mkataba mpya Stamford Bridge na mkataba wa sasa unaisha mwisho wa msimu huu.

Mlinzi huyo amekamilisha vipimo na amemwaga wino wa kuitumikia Los Blancos kwa miaka minne kwa dili yenye thamani ya Euro milioni 6.8 kwa msimu pamoja na bonasi.

Katika dili hiyo Antonio Rudiger na wakala wake Sahr Sensie ambaye ni kaka yake watapata kiasi kikubwa cha pesa ya uhamisho na inakadiriwa watapokea kiasi cha Euro milioni 35 kati yao.

Rudiger amekuwa akiichezea Chelsea tangu mwaka 2017 Julai na ameichezea The Blues michezo 199 katika mashindano yote ambapo amefanikiwa kufunga mabao 12 na kusaidia mengine 7.

SOMA NA HII  WAKATI YANGA WAKIJITAFUTA .....SIMBA YAZIDI KUTAKATA CAF...WAIPITA TP MAZEMBE KWA KILA KITU...

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here