Home Habari za michezo ISHU YA MWAMBUSI KUWA KOCHA MKUU IHEFU IMEKAA HIVI AISEE..KATWILA AFANYIWA YA...

ISHU YA MWAMBUSI KUWA KOCHA MKUU IHEFU IMEKAA HIVI AISEE..KATWILA AFANYIWA YA KAZE NA YANGA….


Baada ya Ihefu kushindwa kupata ushindi kwenye mechi tatu za mwanzo za Ligi Kuu Bara msimu huu, uongozi wa timu hiyo umeamua kumteua Juma Mwambusi kuwa kocha mkuu mpya akichukua nafasi ya Zuberi Katwila atakayesalia kama kocha msaidizi.

Mwambusi aliyekuwa mapumzikoni tangu Januari 2021 alipojiuzulu nafasi ya kocha msaidizi wa Yanga kutokana na sababu za kiafya, ameongezwa kwenye benchi la Ihefu na taarifa kutoka ndani ya timu hiyo atakuwa akishirikiana na watu waliokuwepo kwenye benchi hilo tangu awali akiwemo Katwila.

Ikumbukwe Katwila alijiunga na Ihefu Mwezi Oktoba mwaka 2022 baada ya kuachana na Mtibwa Sugar akichukua mikoba ya Maka Mwalwisi kipindi timu hiyo ikiwa katika hatari ya kushuka daraja lakini alishindwa kuikwamua na kushuka nayo katika msimu wa 2020/2021.

Msimu wa 2021/2022 Katwila aliiongoza timu hiyo kucheza Championship (Zamani Ligi Daraja la Kwanza) na kuibuka bingwa akairudisha tena Ligi Kuu msimu huu akiiongoza kwenye mechi tatu na kupoteza zote, 1-0 mbele ya Ruvu Shooting, 1-0 dhidi ya Namungo  na 3-1 dhidi ya Mtibwa na kuifanya ibuluze mkia kwenye msimamo.

Mwambusi anayesifika kwa ubora wa mbinu na kuwaunganisha wachezaji, mechi yake ya kwanza kuiongoza Ihefu itakuwa Jumanne, Septemba 20 ugenini dhidi ya KMC mchezo utakaopigwa saa 10:00 jioni kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.

Katwila amekuwa kocha wanne kung’oka kwenye kiti cha kocha Mkuu Ligi Kuu tangu kuanza kwa msimu huu baada ya Abdihimid Moallin wa Azam aliyepangiwa majukumu mengine ndani ya kikosi hicho, Zoran Maki wa Simba aliyeondoka kwa makubaliano ya pande zote mbili na Juma Mgunda aliyeondoka Coastal Union na kujiunga Simba kama kocha wa muda.

SOMA NA HII  UONGOZI SIMBA WATOA UFAFANUZI HUU JINSI WATAKAVYOPITA NA UPEPO LIGI YA MABINGWA