Home news STARS YAANZA MAZOEZI LEO UWANJA WA MKAPA,KIBU DENNIS, KIBWANA NDANI

STARS YAANZA MAZOEZI LEO UWANJA WA MKAPA,KIBU DENNIS, KIBWANA NDANI


KIKOSI cha timu ya taifa ya Tanzania,  Taifa Stars leo Oktoba 4 kimeanza mazoezi kwa ajili ya maandalizi ya mchezo wa kuwania tiketi ya kufuzu Kombe la Dunia 2022.

Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa Oktoba 7, Uwanja wa Mkapa ambapo zote zinapambana kusaka tiketi ya kufuzu Kombe la Dunia wakiwa wapo kundi J.

Jonas Mkude hajaripoti kambini kutokana na matatizo ya kifamilia kwa mujibu wa Meneja wa Stars, Nadir Haroub.

Kocha Kim Poulsen ameonekana akiwapa program maalumu wachezaji wote ili kuwaweka sawa kwa ajili ya mchezo huo.

Pia Kibu Denis na Kibwana Shomari ni miongoni mwa wachezaji ambao wameripoti kambini leo na kuanza mazoezi Uwanja wa Mkapa.

SOMA NA HII  KILICHOWATOA MASTAA HAWA YANGA