Home news BAADA YA LIGI KUANZA NA KUONA HALI HALISI…SAKHO NA VARANE WAVUNJA UKIMYA...

BAADA YA LIGI KUANZA NA KUONA HALI HALISI…SAKHO NA VARANE WAVUNJA UKIMYA MSIMBAZI


KIKOSI cha Simba, kinarudi tena kuanza kujifua upya baada ya kurejea kutoka mkoani kwa mechi za Ligi Kuu Bara, ili kujiandaa na mchezo wao wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Jwaneng Galaxy ya Botswana, huku nyota wake wa kigeni, Henock Baka ‘Varane’ na Pape Ousmane Sakho wakivunja ukimya.

Nyota hao walikiri upinzani waliokutana nao kwenye mechi zao za Ligi Kuu Bara zimewafanya waujue ugumu wa ligi hiyo, wakisema ina ushindani mkubwa na kuwapa akili ya kufikiria zaidi.

“Ushindani ni mkubwa mno zaidi ya nilivyowaza hapo awali lakini wala haina shida juu ya hilo mbali ya mbinu za makocha wachezaji tutajiandaa zaidi na nikuhakikishie tutafanya vizuri na tutashinda,” alisema Varane.

Naye Sakho alisema ushindani katika mechi yoyote lazima uwepo lakini ugeni na mazingira ya hapa nchini ameanza kuyaelewa na si muda mrefu atahakikisha anapambana na kutoa mchango zaidi kwa timu yake.

“Simba kuna wachezaji wengi wazuri wanaoweza kwenda kupambania ubingwa wa ligi na kama maelewano yakizidi kuongezeka kati yetu na wale waliokuwa katika kikosi msimu uliopita tutakuwa imara zaidi,” alisema Sakho aliyeshindwa kuendelea na mechi ya Dodoma Jiji.

Kocha Didier Gomes alisema kutokana na mafanikio ya msimu uliopita kwao, imekuwa ni changamoto msimu huu kwa vile timu nyingine zimekuwa zikiwakamia na kucheza kwa nguvu zaidi dhidi yao.

“Mbali ya mazoezi na masuala ya kiufundi ambayo tunayafanya mazoezini ili kushinda nitakuwa na awamu moja ya kuongea na wachezaji wangu kabla ya mechi kujindaa kiakili kile ambacho wanakwenda kukutana nacho kutoka kwa wapinzani,” alisema.

SOMA NA HII  BADO 180 TU YANGA ILIPIZE KISASI KWA SIMBA....ISHU NZIMA IKO HIVI...