Home Uncategorized HII HAPA MITAMBO MINGINE YA MABAO NDANI YA SIMBA

HII HAPA MITAMBO MINGINE YA MABAO NDANI YA SIMBA



SIMBA iliyo chini ya Kocha Mkuu, Sven Vandenbroeck, wachezaji wake wengi walikuwa wameanza kujenga ushkaji na nyavu kabla ya Ligi Kuu Bara kusimamishwa kutokana na janga la Virusi vya Corona.

Hakukuwa na mechi ya ushindani ambayo ilichezwa tangu Machi 17 kutokana na janga la Virusi vya Corona ila kwa sasa kuna matumaini ya ligi kurejea kuanzia Juni 13.

Ikiwa imefunga mabao 63 kibindoni, miongoni mwa wachezaji wake wawili ambao ni viungo ni mitambo ya kutengeneza mabao ambapo wamehusika kwenye mabao 15.

Gerson Fraga ametupia mabao matatu huku mshikaji wake Deo Kanda akiwa ametupia mabao saba na kutengeneza pasi tano za mabao.

Simba ipo nafasi ya kwanza ikiwa na pointi zake 71 kibindoni kwa sasa, kinara wa kucheka na nyavu ni Meddie Kagere mwenye mabao 19 na pasi tano za mabao.

SOMA NA HII  YANGA BILA TSHISHIMBI, KWA SIMBA KUTAKUWA NA TATIZO…