Home Habari za michezo NABI AWACHANA RIVERS UNITED…AWAPANIA HASWAA…AMEZUNGUMZA HAYA

NABI AWACHANA RIVERS UNITED…AWAPANIA HASWAA…AMEZUNGUMZA HAYA

NABI AONGEZEWA MKATABA YANGA...

Kocha Mkuu wa Yanga, Nasreddine Nabi amefunguka kwamba wana timu ambayo inaweza kupambana na yoyote kati ya hizo lakini akasema ungekuwa uwezo wake angeomba wapangwe aidha na Rivers United au USM Alger.

Akizungumza na chombo kimoja cha habari kwa njia ya simu, Nabi amesema anawatamani sana Rivers ili aweze kulipa kisasi kwani waliwahi kumwondoa vibaya msimu wa juzi wa Ligi ya Mabingwa Afrika.

“Nakumbuka ilikuwa ni mwanzo na tulikuwa na changamoto nyingi nadhani hii nafasi tukikutana nao nitafurahi ili nao wajue ubora wetu halisi wa sasa, ukweli lingekuwa ombi langu ningecheza na hawa,” alisema Nabi
Aidha Nabi aliongeza kama sio Rivers basi atafurahi kuwapokea USM Alger,

“Ukikutana na timu za Kaskazini ni jambo zuri kuanzia kwao kisha kumalizia kwetu.”

SOMA NA HII  TAIFA STARS YAFANYA MAJARIBIO KWENYE MECHI MUHIMU..KUACHWA KAPOMBE NA TSHABALALA INASHTUA