Home Uncategorized FEBREGAS AMPA ANGALIZO KIUNGO MPYA WA CHELSEA

FEBREGAS AMPA ANGALIZO KIUNGO MPYA WA CHELSEA


KIUNGO wa zamani wa timu ya Chelsea, Cesc Fabregas amesifu uwezo wa kiungo chipukizi wa timu ya Chelsea Billy Gilmour kwa kusema kuwa akiongeza juhudi atakuwa bora zaidi.

Gilmour alikuwa sehemu ya kikosi kilichoibamiza Liverpool jana Uwanja wa Stamford Bridge kwenye mchezo wa Kombe la FA England wakati timu yake ikishinda mabao 2-0 na kutinga hatua ya robo fainali ya kombe hilo.

Chelsea ilianza kuitungua Chelsea dakika ya 13 kupitia kwa Willian na bao la pili lilipachikwa na Ross Barkely dakika ya 64 licha ya jitihada za Liverpool ya Jurgen Klopp kupambana kupindua meza mambo yalikuwa magumu.

Fabregas amesema, Gilmour ni kiungo mwenye maajabu uwanjani na anamfurahia kumtazama kutokana na uwezo wa kufanya maamuzi na kujiamini katika yale anayofanya.

SOMA NA HII  MTAMBO WA MABAO YA VIWANJA VIGUMU NDANI YA SIMBA KUANZA LEO