Home Uncategorized MTAMBO WA MABAO YA VIWANJA VIGUMU NDANI YA SIMBA KUANZA LEO

MTAMBO WA MABAO YA VIWANJA VIGUMU NDANI YA SIMBA KUANZA LEO


 KOCHA Mkuu wa Simba,Sven Vandenbroeck raia wa Ubelgiji amesema kuwa anaweza kumtumia nahodha wa kikosi hicho John Bocco kwenye kikosi cha leo kitakachomenyana na JKT Tanzania.

 


Bocco katika michezo miwili ya mwanzo ambayo Simba ilianzia katika viwanja vya mikoani alifanikiwa kufunga bao moja kwene ushindi wa mabao 2-1 mbele ya Ihefu kwenye mchezo dhidi ya Mtibwa Sugar wakati Simba ikiambulia sare ya kufungana bao 1-1 alishindwa kucheka na nyavu
.


Sven amesema kuwa amekuwa akifurahishwa na uwezo wa Bocco haswa katika michezo ya mikoani jambo ambalo linampa nafasi ya kucheza kuelekea mchezo wao dhidi ya JKT Tanzania.

“Bocco amekuwa akifanya vizuri katika michezo ambayo tunacheza katika viwanja vya ugenini haswa mikoani,hivyo lazima awe na nafasi ya kucheza kwa kuwa tunafahamu atatupa faida kuelekea mchezo huu.

“Lakini lolote  linaweza kutokea kwa kuwa kuna wachezaji wengi wazuri katika eneo la ushambuliaji ambao pia wanaweza kucheza na kuisaidia timu hii ni faida kubwa sana katika kikosi chetu,lazima tujivunie hilo,”amesema.

Bocco katika michezo miwili iliyopita ya Simba ambayo walicheza jijini Dar es Salam hakupata nafasi ya kucheza ambapo walitumika washambuliaji Meddie Kagere na Chris Mugalu.

Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara alisema kuwa kwa sasa tayari Bocco amesharejea kwenye ubora wake hivyo kuanza kikosi cha kwanza leo Oktoba 4 mbele ya JKT Tanzania ni maamuzi ya mwalimu.
SOMA NA HII  HILI NDILO JEMBE ANALOLIKUBALI KOCHA MKUU WA SIMBA