Home Uncategorized HILI NDILO JEMBE ANALOLIKUBALI KOCHA MKUU WA SIMBA

HILI NDILO JEMBE ANALOLIKUBALI KOCHA MKUU WA SIMBA

Wachezaji wa Klabu ya Namungo  wakiongozwa na Kikoti mwenye jezi namba nane wakiwa kwenye furaha kabla ya Ligi kusimamishwa kupisha maambukizi ya Virusi vya Corona.


KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck amesema kuwa anavutiwa na uwezo wa kiungo anayekipiga ndani ya Namungo FC, Luka Kikoti.

Kikoti amekuwa kwenye ubora wake ambapo kwenye mchezo walipokutana na Simba Uwanja wa Taifa alimtungua bao moja Beno Kakolanya wakati Simba ikishinda kwa mabao 3-2.

Ndani ya Namungo FC, Kikoti anavaa jezi namba nane akiwa uwanjani akishindwa kufunga basi anaweza kutngeneza nafasi ya kufunga.

Sven amesema:”Kikubwa ambacho ninakihitaji kwenye kikosi changu ni kuongeza viungo na hiyo itanifanya nizidi kupata uwanda mpana wa kuchagua kikosi.

“Miongoni wa wachezaji ambao nimeona ni wazuri ni pamoja na yule kiungo wa Namungo, ambaye alifunga pia bao,(Luka Kikoti) yupo vizuri na anajua kile anachokifanya ndani ya uwanja,”.

Kikoti ndani ya Namungo iliyo chini ya Hitimana Thiery ametupia mabao manne na kutoa pasi sita za mabao.

SOMA NA HII  RONALDO WA JUVENTUS AKOSA PENALTI, TIMU YAKE YATINGA HATUA YA FAINALI