Home Uncategorized RONALDO WA JUVENTUS AKOSA PENALTI, TIMU YAKE YATINGA HATUA YA FAINALI

RONALDO WA JUVENTUS AKOSA PENALTI, TIMU YAKE YATINGA HATUA YA FAINALI



CRISTIANO Ronaldo wa Juventus, alikosa penalti kwenye mchezo wa marudiano Kombe la Italia jana mbele ya AC Milan hatua ya nusu fainali. Timu yake imefuzu hatua ya fainali kwa faida ya bao la ugenini.

Kwenye mchezo wa kwanza timu hizo zilitoshana nguvu Uwanja wa San Siro kwa kufungana bao 1-1 Februari.

Licha ya tofauti ya miezi minne kati ya michezo hiyo kupita imeonyesha kuwa na mfanano mkubwa wa matukio ambapo mchezo wa kwanza Ronaldo alifunga baada ya tukio la penalti kutoonekana awali mpaka marudio ya VAR yalipogundua tatizo hilo.

Kwenye mchezo huo Ronaldo alifunga penalti hiyo na kuwafanya walazimishe sare ya kufungana bao 1-1 ambalo limewapa nafasi ya kusonga mbele ila kwenye tukio la jana, licha ya VAR kuamua penalti, Ronaldo alikosa.

Hatua hiyo inaifanya Juventus kuongeza rekodi ya kutinga fainali ikiwa ni mara 19 na timu ya pili ni Roma iliyotinga mara 16.

SOMA NA HII  SIMBA YATOA NENO KWA WATANZANIA