Home Uncategorized MTAMBO WA KAZI WAUNGANA NA WENZAKE NDANI YA KIKOSI CHA AZAM FC

MTAMBO WA KAZI WAUNGANA NA WENZAKE NDANI YA KIKOSI CHA AZAM FC


BEKI wa Azam FC, Nicolas Wadada jana ameungana na wachezaji wenzake kufanya mazoezi ya pamoja kwa ajili ya maandalizi ya mchezo wa kesho dhidi ya Mbao FC.

Wadada alikuwa nchini Uganda baada ya Serikali kusimamisha masuala ya michezo kutokana na janga la Virusi vya Corona.

Tangu Machi 17, hakukuwa na mechi ya ushindani kwa kipindi hicho cha kuchukua tahadhari, ila kwa sasa Serikali imeruhusu masuala ya michezo kuendelea huku tahadhari ikichukuliwa kwa kuwa bado janga la Corona lipo.

 Azam FC ilianza mazoezi Mei 27 ila Wadada hakuwa ndani ya kikosi kwa kuwa mipaka ya Uganda imefungwa kuchukua tahadhari dhidi ya Corona.

Inaelezwa kuwa Wadada ametua Bongo kwa ndege binafsi ya Azam FC ili kuendelea kutimiza majukumu ndani ya kikosi hicho kilicho chini ya Aristica Cioaba.

SOMA NA HII  DROO YA LIGI YA MABINGWA ULAYA IPO NAMNA HII