Home Uncategorized SIMBA YAZITAKA POINTI TATU ZA RUVU SHOOTING

SIMBA YAZITAKA POINTI TATU ZA RUVU SHOOTING


LUIS Miquissone, kiungo mshambuliaji wa Simba amesema
mazoezi waliyofanya kwa muda wa wiki mbili yatawasaidia kupata matokeo chanya mbeke ya Ruvu Shooting.

Kesho Juni 14, Simba itamenyana na Ruvu Shooting Uwanja wa Taifa ikiwa ni mchezo wa Ligi Kuu Bara.

Raia huyo wa Msumbiji amesema kila kitu kipo sawa na wataingia uwanjani kwa kupambana kwa kuwa walikosa mechi ya ushindani kwa muda mrefu.

“Tupo tayari kwa ushindani na mchezo nina amini utakuwa mgumu, kikubwa mashabiki wajitokeze kuona burudani kwani tulishindwa kutoa burudani kwa muda mrefu,”.

Simba ipo nafasi ya kwanza ikiwa na pointi 71 baada ya kucheza mechi 28, imetupia mabao 68.

SOMA NA HII  WANNE WATAJWA KUONDOKA SIMBA