Home Uncategorized WANNE WATAJWA KUONDOKA SIMBA

WANNE WATAJWA KUONDOKA SIMBA


Imeelezwa kuwa uongozi wa klabu ya Simba umepanga kuwatoa kwa mkopo nyota wake watatu akiwamo mshambuliaji, Adam Salamba, anayekwenda kukipiga nchini Ureno.

Taarifa imeeleza kuwa Salamba ambaye alisajiliwa na Simba msimu huu akitokea Lipuli FC kwa dau la Sh milioni 40.

Mchezaji huyo amekosa namba ya kudumu katika kikosi hicho cha Msimbazi kinachonolewa na kocha, Patrick Aussems, kutokana na kushindwa kumudu ushindani uliopo.

Adha taarifa imesema uwepo wa washambuliaji hatari kikosini hapo kama vile Meddie Kagere, John Bocco na Emmanuel Okwi, ulikuwa ni sababu tosha kwa Salamba kushindwa kutamba ndani ya Wekundu hao wa Msimbazi.

Taarifa kutoka ndani ya Simba zinaeleza kuwa wachezaji wengine ambao wanatarajiwa kutolewa kwa mkopo ni Rashid Mohammed, anayekwenda nchini Kenya na Abdul Mohammed, ambaye haijajulikana atakwenda timu gani.

Aidha, chanzo hicho kilieleza kwamba, tayari Aussems amekabidhi ripoti yake kwa uongozi inayoonyesha wachezaji watakaoachwa lakini hakuwataja kwa majina.

Hata hivyo, mtoa taarifa huyo alisema alichoeleza kocha ni kwamba wataachwa wachezaji wanne wa kigeni na watatu wazawa.

SOMA NA HII  KOCHA SIMBA AITOA TIMU YAKE KWENYE MICHUANO YA KIMATAIFA