Home Uncategorized SABABU YA YANGA KUPANDA NDINGA MPAKA SHINYANGA HII HAPA

SABABU YA YANGA KUPANDA NDINGA MPAKA SHINYANGA HII HAPA


INAELEZWA kuwa sababu kubwa iliyowafanya wachezaji wa Yanga kuelekea Shinyanga kwa ndiga ni kuepusha gharama zisizo za lazima pamoja na kuwaweka wachezaji kwenye mazoezi kwa wakati.

Yanga ilisepa Dar, Juni 10 kwa basi la timu kuelekea Shinyanga ambapo leo Juni 13 watcheza mchezo wa ligi dhidi ya Mwadui FC Uwanja wa Kambarage.
Habari zinaeleza:-“Sababu iliyowafanya Yanga kwenda na ndege ni tahadhari dhidi ya Corona, kwani iliwapasa wasafiri mafungumamafungu jambo ambalo lingegharimu gharama na ukizingatia kwamba kama fungu la mwisho lingefika Ijumaa, wachezaji wasingepata muda wa kufanya maandalizi ya mechi yao” ilieleza taarifa hiyo.
Ofisa Habari wa Yanga, Hassan Bumbuli ambaye alisema kuwa wanamshukuru Mungu kwa kuwa wamefika Shinyanga salama na kuwaepusha kwenye ajali.
“Tulipata ajali maeneo ya Manyoni karibu kabisa na kufika Singida na basi lilikuwa kwenye spidi, tairi moja lilipasuka, Mungu alimuongoza dereva ambapo tulitembea zaidi ya mita 1,000 mpaka gari likasimama ili tufanyie matengenezo.
“Halikuwa jambo jema kwani hakuna ambaye anapanga ajali ila tunashukuru wote tupo salama na tunaendelea kujipanga kwa ajili ya masuala mengine, mashabiki waendelee kutupa sapoti,” amesema Bumbuli. 
Kocha Mkuu wa Yanga, Luc Eymael jana Juni 12 aliwasili Shinyanga akiwa na mshambuliaji wao namba moja David Molinga mwenye mabao nane. 
SOMA NA HII  AZAM FC WAIBUKIA HUKU KWA SASA WAOMBA SAPOTI YA MASHABIKI WAO