Home Habari za michezo BENCHIKA KUSTAAFU SIMBA?…HAKUBALI KUHARIBU CV YAKE…TIMU ALIYOPITA ALISTAAFU

BENCHIKA KUSTAAFU SIMBA?…HAKUBALI KUHARIBU CV YAKE…TIMU ALIYOPITA ALISTAAFU

Habari za Simba leo

Kwa miaka kadhaa sasa nimekuwaa nikifatilia soka la Bara la Afrika na moja ya watu ambao ninawafahamu na wenye heshima kwenye soka la Afrika ni Abdelhak Benchikha Mwamba huyu kutokea nchini Algeria.

Tabia ninayoifahamu Kwa bwana Benchikha ni kocha mwenye msimamo asiyekubali CV yake kuchafuliwa hovyo hovyo na kocha mzuri endapo utamtimizia nahitaji na atakupa mafanikio kwelikweli.

Mfano ni mwaka 2022 pale klabu ya RS Berkane iliposhindwa kumtimizia mahitaji yake wakati wa dirisha la usajili hakusita kufanya maamuzi magumu na kuondoka kwenye klabu hiyo.

Hata sababu ya yeye kuondoka USM Alger ni pale mashabiki wa timu hiyo walipomuonyesha dharau aliamua kukaa kando huyu ndiye Abdelhak Benchikha ninaemfahamu mimi.

Huyu jamaa ni kama Jose Mourinho huwa hachelewi kuzungumzaaa kwenye vyombo vya Habari kama alivyofanya jana endapo wachezaji au uongozi wa klabu anayoifundisha watamvuruga.

Uhalisia ni kweli endapo viongozi wa Simba SC watashindwa kumpa kile anachokihitaji wakati wa dirisha kubwa hatosita kufanya maamuzi magumu ya kung’atuka ndani ya kikosi hicho.
Kocha Benchikha amesema haya baada ya mechi.

“Tangu nimeanza kufundisha mpira sikuwai kukutana na timu yenye
wachezaji wagumu kuelewa kama hii simba timu inacheza tofauti kabisa na matakwa yangu.

“Nitaongea tena na viongozi wangu kama nitakubaliwa kuunda timu yangu upya msimu ujao ili niandae list yangu ya wachezaji nitakaoweza kuunda timu bora Africa.

“Ila kama watashindwa kukubaliana na mimi basi watambue kuwa CV yangu sijaitengeza na pesa nashuka CV yangu kila kukicha naweza kufanya maamuzi sahihi,” amesema Benchikha.

SOMA NA HII  TIMU HIZI KUIPA UBINGWA YANGA...GUEDE AENDELEZA MAAJABU AFANYA HAYA