Home Uncategorized JEMBE JIPYA LA YANGA KUTUA KUANZA KAZI,NI MTAMBO WA MABAO

JEMBE JIPYA LA YANGA KUTUA KUANZA KAZI,NI MTAMBO WA MABAO

 


UONGOZI wa timu ya Yanga umesema kuwa unatarajiwa kumpokea mshambuliaji wao mpya Sadio Ntibazonkiza mara baada ya kumalizika kwa mapumziko ya mechi za timu za taifa zinaoendelea kufanyika duniani kote.

 

Ntibazonkiza mwenye uraia wa Burundi alisajiliwa na Yanga Oktoba 12 akiwa na timu ya taifa ya Burundi ilipokuja kucheza na timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars ambapo mchezaji huyo aliifungia timu yake bao pekee ambapo Burundi walishinda kwa bao 1-0.

 

 Ofisa Muhamasishaji wa Yanga, Antonio Nugaz, amesema kuwa kiungo huyo kwa sasa yupo katika majukumu ya timu ya taifa ya Burundi na mara baada ya kumalizika michezo hiyo atakuja kujiunga rasmi na Yanga tayari kwa kuanza kucheza.

 

“Ntibazonkiza kama ambavyo tuliwataarifu awali kuwa atarejea nchini mara baada ya kufunguliwa kwa dirisha dogo la usajili, kwa sasa yupo kwenye kambi ya timu ya taifa ya Burundi hivyo baada ya kumaliza majukumu ya timu ya taifa atakuja rasmi kujiunga na kambi ya Yanga.

 

“Ujio wa Ntibazonkiza ni ongezeko la mchezaji mwenye uzoefu kwenye kikosi chetu jambo ambalo naamini litatusaidia kuhakikisha tunazidi kufanya vizuri kwenye michezo yetu ya ligi,”amesema kiongozi huyo.


 Kwenye mchezo wa Burundi na Maurtania uliochezwa Novemba 11, ulikamilika kwa sare ya kufungana bao 1-1 ambapo nyota huyo alifunga bao la kusawazisha kwa mpira wa faulo na watarudia Novemba 15 na hivyo Novemba 16 staa huyo ataanza safari ya kutua nchini.

SOMA NA HII  KAPOMBE: NIMERUDI SASA NI KAZI JUU YA KAZI KITAIFA NA KIMATAIFA