Home Uncategorized LEO KAZI KAZI, VIWANJA VIWILI KUWAKA MOTO

LEO KAZI KAZI, VIWANJA VIWILI KUWAKA MOTO


LEO Juni 13, viwanja viwili vitakuwa na kazi ya kukupambana na mihimili ya miguu 44 baada ya masuala ya michezo kuruhusiwa kuendelea na Serikali.
Hakukuwa na mechi ya ushindani kwenye ligi tangu Machi 17 na sababu kubwa ilikuwa ni janga la Virusi vya Corona ambalo lilivurugavuruga dunia.
Kwa sasa tayari Serikali imeridhia masuala ya michezo kuendelea huku ikiwataka mashabiki na wadau kuendelea kuchukua tahadhari dhidi ya Corona kwa kuwa bado ipo.
Mechi mbili zitachezwa leo ambapo, Yanga itakutana na Mwadui FC Uwanja wa Kambarage huku Coastal Union ikimenyana na Namungo FC, Uwanja wa Mkwakwani.
Charles Mkwassa, Kocha Msaidizi wa Yanga amesema kuwa wapo tayari kwa ajili ya mchezo huo wana imani watapata matokeo.
Kwa upande wa mchezo wa Namungo dhidi ya Coastal Union, Juma Mgunda Kocha Mkuu wa Coastal Union alisema kuwa utakuwa ni mchezo mgumu ila wapo tayari kubaki na pointi tatu huku Hitimana Thiery wa Namungo akisema kuwa watawashangaza wengi.
SOMA NA HII  TRY AGAIN AWAKUMBUSHA WATANZANIA JAMBO HILI MUHIMU SIMBA VS AL AHLY