Home Uncategorized HIVI NDIVYO YANGA ILIVYOBANWA MBAVU NA WAJELAJELA JANA TAIFA

HIVI NDIVYO YANGA ILIVYOBANWA MBAVU NA WAJELAJELA JANA TAIFA

KIKOSI cha Yanga jana kimebanwa mbavu kwenye Uwanja wa Taifa mbele ya wajelajela Tanzania Prisons kutoka Mbeya kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara kwa kulazimisha sare ya bila kufungana.
Yanga iliyo chini ya Luc Eymael ambaye ni Kocha Mkuu walianza mpira kwa kasi kuliandama lango la Prisons ila uimara wa mlinda mlango Jeremiah Kisubi ulivuruga mipango ya washambuliaji wa Yanga wakiongozwa na Bernard Morrison.
Morrison ambaye alicheza mchezo wa jana kibabe alikwama kupeleka furaha jangwani kwani dakika ya 72 alipaisha penalti baada ya mwamuzi kutafsri kuwa amechezewa faulo na mlinda mlango Kisubi ambaye alionyeshwa kadi ya njano.
Sare hiyo iliwafanya Yanga watoke kinyonge uwanja wa Taifa wakiwa wamecheza jumla ya mechi 20 na kujiwekea kibindoni pointi 39.
Mchezo wa kwanza waliocheza Uwanja wa Samaora, Yanga iliibuka kidedea kwa kushinda bao 1-0 na ilipokutana nao kwenye mchezo wa Kombe la Shirikisho Yanga iliwafunga mabao 2-0 ambapo Morrison alifunga bao lake la kwanza kwa mkwaju wa penalti kwa Yanga.

SOMA NA HII  ZAHERA AITAFUTA REKODI YA KOCHA SIMBA CAF