Home Habari za michezo VITA VIPYA NDANI YA SIIMBA…BALEKE VS PHIRI HAPATOSHI

VITA VIPYA NDANI YA SIIMBA…BALEKE VS PHIRI HAPATOSHI

Habari za Simba

Mshambuliaji kutoka nchini Zambia na Klabu ya Simba SC, Moses Phiri ametangaza dhamira ya kurejea katika mpango wa kuisaidia klabu hiyo ya Msimbazi, baada ya kupona kutoka katika majeraha ambayo yalikuwa yakimsumbua tangu mwishoni mwa mwaka 2022.

Phiri ameshindwa kupata nafasi ya kucheza ndani ya Kikosi cha Simba SC mara kwa mara tangu alipopona jeraha lake la Mguu, ambapo kocha Roberto Oliviera amekuwa akimtumia Jean Baleke katika eneo la ushambuliaji.

Mshambuliaji huyo aliyesajiliwa Simba SC mwanzoni mwa msimu huu 2022/23 akitokea kwao Zambia alikokuwa akiitumikia Zanaco FC,

amesema anaamini bado ana nafasi ya kurejea katika kikosi cha kwanza na kuisaidia Simba SC katika kipindi hiki, ambacho inawania Ubingwa wa Tanzania Bara na kusaka nafasi ya kucheza Nusu Fainali Ligi ya Mabingwa Barani Afrika.

“Kila kitu ni mipango ya mwalimu kuhusiana na mimi kucheza au kutokucheza ndani ya Simba SC, naamini nitacheza tu.”

“Unajua nilikuwa majeruhi kwa muda mrefu hivyo lazima nijipange vyema kwa ajili ya kuhakikisha kuwa nacheza na naisaidia Simba SC kufanya vyema kwa kufunga mabao ya kutosha kama ilivyokuwa hapo awali.”

“Ninafuraha kuwa Simba, ni timu kubwa ambayo ina malengo makubwa, ukiwa hapa mchezaji lazima uwe unawaza vitu vikubwa ili kuendana na Simba,” Amesema Phiri

Hadi anapata majeraha ya Mguu katika mchezo dhidi ya Kagera Sugar, Moses Phiri alikua ameshaifungia Simba SC mabao 10 na amekuwa katika orodha ya wafungaji Bora msimu huu, akitanguliwa na Fiston Maleye wa Young Africans mwenye mabao 15.

SOMA NA HII  SIMBA KIMEUMANA...KOCHA ATEMA CHECHE HATARI...YANGA WATAJWA