Home Simba SC MANULA AANDIKA REKODI YA DAKIKA 180 AFRIKA, CAF YAMJAZA SIFA

MANULA AANDIKA REKODI YA DAKIKA 180 AFRIKA, CAF YAMJAZA SIFA


MLINDA mlango wa kikosi cha klabu ya Simba, Aishi Manula ameandika rekodi ya kipekee katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika msimu huu baada ya kufanikiwa kusimama langoni katika michezo miwili bila kuruhusu bao lolote yaani ‘Clean Sheet’.

Juzi katika dimba la Mkapa jijini Dar es Salaam, Manula alifanikiwa kuonyesha kiwango bora, huku pia akiokoa mchomo wa hatari katika dakika za nyongeza kwa kupangua shuti kali la Mohammed Sherif.

Uwezo aliouonyesha Manula uliwakuna wengi ambapo Shirikisho la Soka Afrika (CAF), kupitia akaunti yao rasmi ya mtandao wa kijamii waliweka kipande cha video ya Manula akiokoa hatari hiyo na kuandika: “Kuna Aishi Manula mmoja tu. Na anacheza klabu ya Simba ya Tanzania.

“Namna bora ya uokozi inayoipa Simba ushindi dhidi ya mabingwa watetezi wa Ligi ya Mabingwa Afrika Ahly,” 

Kuhusiana na ushindi huo, Manula amesema: “Kwanza tunashukuru kwa kupata pointi tatu muhimu katika mchezo wa jana (juzi) dhidi ya Al Ahly, haikuwa kazi rahisi tulicheza na timu ngumu na bora Afrika lakini jambo la muhimu ni kwamba tulipambana kwa dakika zote 90.

“Malengo yetu ni kuhakikisha tunapambana kufikia malengo tuliyojiwekea msimu huu, ya kufika angalau nusu fainali, tunajua siyo kazi rahisi lakini tutaendelea kupambana,”

SOMA NA HII  HUKU CAF WAKIZIDI KUIMWAGIA MAPESA....SIMBA WAAMUA KUJA NA HILI JIPYA MJINI....